• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufunga breki kunasababisha uchafuzi wa hewa

    (GMT+08:00) 2017-03-15 18:27:26

    Siku hizi magari mengi zaidi yasiyotoa hewa chafu yanauzwa sokoni, lakini watafiti wana wasiwasi kwamba magari bado yanaweza kusababisha uchafuzi.

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Georgia wametoa ripoti kwenye gazeti la sayansi na teknolojia za mazingira wakisema wakati madereva wanapofunga breki, msuguano kati ya vipuri unasababisha chembe ndogondogo za metali zikiwemo shaba, chuma na manganese kuingia hewani, na chembe hizi zinaunganishwa na kemikali ya Sulfate hewani, na kuunda kemikali zinazodhuru zaidi afya ya watu.

    Watafiti wamesema mwanzoni ni vigumu kwa chembe hizi ndogondogo za metali zisizoweza kuyeyuka majini kuingia mwilini mwa binadamu, lakini viwanda vya kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe vimetoa kemikali ya Sulfate hewani, na chembe za metali zikiunganishwa na Sulfate, zitabadilika kuwa kemikali zinazoweza kuyeyuka majini, na watu wanapopumua, ni rahisi kwa kemikali hizi kuingia mwilini.

    Msuguano kati ya vipuri vya magari si chanzo pekee cha chembe ndogondogo za metali, vifaa vya kuteketeza takataka pia vinazalisha chembe hizi.

    Watafiti wanasema hata tukitumia magari yanayotumia nishati ya umeme, utoaji wa chembe za metali hautapungua, hivyo watu wanapotafiti njia za kupunguza uchafuzi wanatakiwa kufikiria jambo hili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako