• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia:Mfumko wa uchumi wapanda hadi asilimia 7.8

    (GMT+08:00) 2017-03-15 19:35:54

    Mfumko wa uchumi nchini Ethiopia umepanda hadi asilimia 7.8 Mwezi Februari.

    Kwa mujibu wa wizara ya biashara nchini humo,hali hiyo imesababishwa na kupanda kwa bei ya chakula haswa mboga na nafaka.

    Waziri wa masuala ya biashara Aled Ziad ameonya wakulima na wafanyibiashara dhidi ya kupandisha bei ya vyakula na mazao yao.

    Wiki hii,bei ya tomato,pilipili na kabeji zimeongeza bei mara tatu .

    Sekta ya kilimo imeathirika nchini Ethiopia kutokana na ukame ulioshuhudiwa mwaka jana ambao umeathiri nchi nyingi za Afrika.

    Shirika kuu la chakula duniani FAO wiki hii limetangaza kwamba zaidi ya nchi nane duniani zinakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame hali ambayo imesababisha mfumko wa uchumi katika nchi nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako