• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Romelu Lukaku akataa kusaini mkataba na klabu ya Everton

    (GMT+08:00) 2017-03-16 09:21:55
    Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amekataa mkataba wenye faida kubwa kwake katika historia ya klabu hiyo.

    Klabu hiyo ya ligi ya Uingereza ilikuwa na matumaini kuwa mchezaji huyo wa Ubelgiji ataingia kwenye mkataba wa miaka mitano unaoaminika kugharimu pauni 140,000 kwa wiki. Wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, Mino Raiola alisema mteja wake alikuwa na uwezekano wa asilimia 99.9 kusaini mkataba mpya katika uwanja wa Goodison Park.

    Lakini Lukaku ameiambia klabu hiyo kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba ambao umesalia miaka miwili kukamilika. Lukaku hajaficha kuhusu mpango wake wa kutaka kusakata kabumbu katika vilabu bingwa Ulaya na amehusishwa na uhamisho wa kurudi katika klabu yake ya zamani Chelsea, ambapo alijiunga na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28 mwaka 2014.

    Ombi la mkataba wa Everton bado lipo wazi huku klabu hiyo ikisema majadiliano zaidi huenda yakafikia makubaliano. Kwa sasa Lukaku hajakubali mkataba wowote, na Everton huenda ikampa kitita cha pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo aliyefunga mabao 19 msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako