• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya maziwa ya Brookside yaongeza bei ya kununua maziwa gafi kwa asilimia 13

    (GMT+08:00) 2017-03-16 19:37:19

    Kampuni ya kusindika maziwa ya Brookside nchini Kenya imeongeza bei ya kununua maziwa gafi kwa asilimia 13.

    Brookside sasa inanunua bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima kwa shilingi 42 kwa lita moja.

    Kampuni nyingine ya maziwa KCC nayo inanunua kwa shilingi 40 huku nayo makapuni mengine yakinunua kwa kati ya 37 na 40.

    Kuongezwa kwa bei hiyo kumechangiwa na kupungua kwa maziwa hali ambayo pia imepelekea kupanda kwa bei ya maziwa yaliosindikwa hadi shilingi 50 hadi 60 kwa nusu lita.

    Brookside ndio yenye mgao mkubwa wa soko ikiwa sasa na asilimia 44.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako