• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Neymar ashinda kesi ya madai kukwepa kulipa kodi

    (GMT+08:00) 2017-03-17 09:05:48

    Mahakama ya rufaa nchini Brazil imetupilia mbali mashtaka ya madai yaliyokuwa yanamkabili mchezaji wa Barcelona pamoja na timu ya Taifa Brazil Neymar Jr. Hatua hiyo imekuja baada ya wakaguzi wa mahesabu kushindwa kuthibitisha dai la mchezaji huyo kutakiwa kulipa kodi ya mapato kiasi cha euro milioni 27.5 badala ya kiasi alicholipa.

    Vile vile Mahakama hiyo imempa uhuru Neymar Jr kuruhusiwa kutumia picha zake za matangazo kusimamiwa na kampuni za familia yake.

    Mwaka 2015, Neymar alishtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi ya zaidi ya euro milioni 63 zilizotokana na mapato yake katika vilabu vya Santos na Barcelona na matangazo kati ya mwaka 2011 na 2014.

    Kwa ushindi huo wa awali, Neymar anapaswa kulipa nusu ya kiasi cha euro milioni 200 anachodaiwa na maafisa wa kodi hata kama atashindwa madai mengine yaliyobaki dhidi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako