• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji 30 kutoka Afrika wauawa katika shambulizi la anga kwenye pwani ya Yemen

    (GMT+08:00) 2017-03-17 18:25:41

    Wahamiaji 30 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika shambulizi la anga lililotuhumiwa kufanywa na helikopta za jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia kwenye boti waliyokuwa wakisafiria katika pwani ya Yemen.

    Duru za usalama zimesema, wengi wa wahamiaji hao walikuwa wakirejea kwa hiari kutoka Yemen na kuelekea nchini Sudan, Somalia, na nchi nyingine za Afrika. Na wahamiaji wengine wengi walifanikiwa kutoroka baada ya shambulizi hilo na wameokolewa.

    Duru nyingine zinasema, idadi kubwa ya wavuvi wa Yemen wameuawa wakati helikopta hiyo iliposhambulia boti yao karibu na pwani ya Bahari Nyekundu ya Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako