• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa nchi inayotoa nafasi nyingi zaidi za ajira barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-18 18:52:37

    China imetoa karibu nafasi 30,000 za ajira barani Afrika katika miaka miwili iliyopita, kiasi hicho kinaongoza nchi nyingine duniani. Hayo yamesemwa na Bwana Jeremy Steven ambaye ni mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Standard Group.

    Bw. Jeremy ameeleza kuwa China inashika nafasi ya saba kwa idadi ya miradi Barani Afrika lakini inatoa ajira nyingi zaidi hali ambayo haikutarajiwa na watu wengi.

    Akitolea mfano Kenya, kwa mujibu wa utafiti wa sera za kazi iliyotolewa na Benki ya Dunia mwezi Machi mwaka jana, China ilikuwa katika nafasi ya tano katika kutoa ajira kati ya mwaka 2003 na 2015 kwa njia ya uwekezaji wake kigeni wa moja kwa moja nchini Kenya.

    wakati wa ziara yake ya nchi tano barani Afrika mwezi Januari mwaka huu, waziri wa wa mambo ya nje wa China Bwana Wang Yi alisema licha ya kudorola kwa uchumi wa dunia na ukuaji biashara, ushirikiano wa viwanda kati ya China na Afrika umekua kwa kasi huku makampuni mengi ya China yakiwekeza barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako