• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Chelsea yazidi kupaa, Arsenal yachapwa

    (GMT+08:00) 2017-03-20 09:29:14

    Huko Britannia Stadium, Vinara wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea wameifunga Stoke City 2-1 na kuendelea kupaa kileleni mwa Ligi hii wakiwa Pointi 13 mbele.

    Bao za Chelsea zilifungwa Dakika za 13 na 87 kupitia Willian na Gary Cahill na lile la Stoke kupachikwa Dakika ya 38 kwa Penati ya Jonathan Walters.

    Timu ya Arsenal mambo yanazidi kuwawia vigumu baada ya kukubali kipigo cha goli 3-1 toka kwa West Bromwicha Albion huko Hawthorns. Kipigo hicho ni cha 4 katika mechi zao 5 za ligi hiyo.

    Bao za West Bromwicha zilipifungwa na Craig Dawson, Bao 2, dakika za 12 na 75, na la Hal Robson-Kanu dakika ya 75 wakati Arsenal wakipata bao la kufuitia machozi dakika ya 15 kupitia kwa Alexis Sanchez.

    Mechi nyingine ilikuwa kati ya Manchetser City dhidi ya Liverpool huko Etihad. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1. Katika mechezo mwingine wa ligi hiyo, Manchester United nayo imeibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Middlesbrough, huku Tottenham Hotspur imeifunga Southampton 2-1.

    EPL sasa inasimama kupisha mechi za kimataifa zilizo kwenye kalenda ya FIFA, itarejea tena April 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako