• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 16 wafariki baada ya kuangukiwa na mti nchini Ghana

    (GMT+08:00) 2017-03-20 10:35:28

    Zaidi ya watu 16 wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na mti mkubwa katika maporomoko ya maji huko Kintampo kwenye jimbo la Brong Ahafo, nchini Ghana.

    Kamanda mkuu wa polisi eneo la Kintampo Bw Desmond Boampong amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusema wengi wa wahanga ni wanafunzi wa sekondari ya juu waliokuwa wakitalii na kuogelea kwenye eneo la tukio.

    Hivi sasa majeruhi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu, na askari wa zima moto na polisi wanaendelea kuokoa watu wanaokwama chini ya mti huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako