• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanasayansi wagundua mabaki ya uyoga yenye historia ndefu zaidi

  (GMT+08:00) 2017-03-20 14:44:00

  Kikundi kinachoundwa na wanapaleontolojia wa China, New Zealand na Marekani kimegundua mabaki nanne ya uyoga yenye historia ya miaka milioni 100. Mabaki hayo yamehifadhiwa vizuri ndani ya karahabu zilizoundwa katikati ya kipindi ambacho miamba ya chaki ilitumbika.

  Kiongozi wa kikundi hicho ambaye pia ni mtafiti wa taasisi ya panleontolojia ya Nanjing Bw. Huang Diying amesema uyoga una maisha mafupi na ni laini, hivyo ni vigumu kubaki alama udongoni, na mabaki yote ya uyoga yaliyogunduliwa yamehifadhiwa ndani ya karahabu.

  Kabla ya hapo, wanasayansi waligundua karahabu moja tu yenye mabaki ya uyoga yenye historia ya miaka milioni 100, lakini mabaki ya uyoga huo hayako kamili na ni vigumu kwa wanasayansi kutafiti historia ya uyoga kupitia mabaki hayo. Hivyo watafiti wamekusanya karahabu zaidi ya elfu 20 zenye mabaki ya uyoga, na kuchagua nne zenye mabaki kamili.

  Watafiti wamegundua uyoga wa kale una sura inayofanana na ile ya kisasa, una urefu wa milimita 2 hadi 3, na unaweza kugawanywa katika aina nne.

  Aidha, watafiti pia wamegundua mabaki ya wadudu waliokula uyoga kwenye karahabu zenye historia ya miaka milioni 125. Hii inamaanisha kuwa uyoga ulianza kuwepo duniani mapema sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako