• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Zanzibar yahepa kukatiwa umeme

    (GMT+08:00) 2017-03-20 19:37:24
    Serikali ya Zanzibar imelipa 10bn / - kupunguza deni ya sh 121bn wanayo daiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika ada za umeme.

    Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo alithibitisha jijini Dar es Salaam jana kuwa serikali ya Zanzibar imelipa fedha hizo katika jitihada za maliza madeni yake kwa TANESCO na kuahidi kuendelea kulipa mpaka deni lote likamilike.

    Malipo haya ya Zanzibar yamekuja siku chache baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli kuamuru usimamizi wa TANESCO kukata umeme kwa watu wote ambao hawalipi bili zao za umeme, ikiwa ni pamoja na serikali ya Zanzibar.

    Alisisitiza kwamba taasisi zote za umma lazima wa malize kulipa madeni yao au kukatiwa umeme.

    Aidha alisema serikali ya Zanzibar peke yake, kupitia shirika la umeme la Zanzibar (ZECO), inadaiwa sh 121bn .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako