• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 16 wamejeruhiwa kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-03-21 09:59:00

    Ndege ya abiria ilianguka na kuungua katika uwanja wa ndege wa Wau, Sudan Kusini alasiri ya jana na kusababisha watu 16 kujeruhiwa.

    Waziri wa habari wa jimbo la Wau, Bona Gaudenesio amethibitisha kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa na watu 49, na kusema idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo bado haijulikani. Hivi sasa, kazi ya uokoaji bado inaendelea.

    Habari zinasema, walinzi wa amani wa China walioko karibu na eneo la tukio wamekwenda moja kwa moja kushiriki kwenye kazi ya uokoaji na kusaidia kuzima moto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako