• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikundi cha Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing chashinda kwenye mashindano ya droni

  (GMT+08:00) 2017-03-23 07:03:52

  Fainali ya mashindano ya roboti ya kimataifa ya Mohamed Ben Zayed ambayo ni moja kati ya mashindano muhimu ya kimtaifa ya droni na roboti ilifanyika tarehe 15 hadi 19 Machi huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.

  Vikundi 143 kutoka nchi na sehemu 35 duniani vikiwemo vikundi vya Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachusetts na Chuo Kikuu cha Pennsylvania vimeshiriki kwenye mashindano hayo. Vikundi vilivyoshiriki kwenye mashidano hayo vilitakiwa kusanifu droni na magari yasiyo na madereva ambayo yanaweza kushirikiana kumaliza kazi maalum katika hali ya dharura. Baada ya duru tatu za mashindano, vikundi 26 viliingia fainali, vikiwemo vikundi viwili kutoka China.

  Vikundi hivi viwili ni pamoja na vikundi kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing na Chuo Kikuu cha safari ya ndege na ya anga ya juu cha Beijing.

  Mwishowe kikundi cha Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing kilipata ushindi katika mradi wa kusanifu droni inayoweza kuruka na kutua yenyewe na kuchunguza shabaha inayohamahama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako