• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu za pole kwa Malkia wa Uingereza kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea mjini London

    (GMT+08:00) 2017-03-23 17:22:22

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za pole kwa Malkia Elizabeth wa Uingereza kufuatia shambulizi la kigaidi lillilotokea mjini London.

    Rais Xi amelaani vikali shambulizi hilo na kutoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa watu waliofariki dunia katika shambulizi hilo, pia ametoa pole kwa majeruhi wa tukio hilo.

    Rais Xi amesema ugaidi ni adui mkubwa wa jumuiya ya kimataifa, na China inapinga aina zote za ugaidi. Ameongeza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano na Uingereza na jumuiya ya kimataifa, na kufanya juhudi ili kulinda usalama wa China, Uingereza na dunia kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako