• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa jibu kwa kauli kuhusu "Bahari ya Kusini"

    (GMT+08:00) 2017-03-23 19:07:43

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, hivi sasa mwelekeo wa hali ya eneo la Bahari ya Kusini ni mzuri, na kwamba Japan inakusudia kueneza habari zisizo za kweli kuhusu tishio la China ili kujiongezea zana za kijeshi.

    Hua amesema hayo kutokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na maofisa wa Japan kuhusu hali ya Bahari ya Kusini ya China. Pia amesisitiza kuwa kutokana na chanzo cha kihistoria, jumuiya ya kimataifa hususan nchi jirani za Asia siku zote zinafuatilia mwelekeo wa kijeshi wa Japan. Amesema China ina haja ya kuchukua tahadhari kubwa juu ya hatua na makusudio halisi ya Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako