• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshukiwa aliyeuawa wa shambulizi London atambuliwa

    (GMT+08:00) 2017-03-24 09:55:02

    Polisi mjini London wametoa taarifa ikisema mshukiwa wa shambulizi la kigaidi mjini London ametajwa kuwa ni Khalid Masood, mzaliwa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 52.

    Msemaji wa polisi amesema Masood amewahi kutuhumiwa kumiliki silaha bila idhini na kuharibu utaratibu wa umma, na kabla ya tukio la jana polisi hawakuwa na habari zozote za kijasusi kuhusu shambulizi hilo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw Boris Johnson ambaye yuko ziarani mjini New York Marekani amesema wahanga wa shambulizi la Westminster wanatoka nchi 11, na kulitaja shambulizi hilo kama shambulizi dhidi ya dunia nzima.

    Pia ametoa mwito kwa makampuni ya internet na mitandao ya kijamii kuchukua hatua kuondoa habari zenye msimamo mkali ili kuepuka watumiaji wa Internet wasiathiriwe na habari hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako