• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Australia wakutana

    (GMT+08:00) 2017-03-24 17:46:22

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amekutana na waziri mkuu wa Australia Bw. Malcolm Turnbull, ikiwa ni mara ya tano kwa mawaziri hao kukutana.

    Katika mazungumzo yao, Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kushughulikia vizuri kazi ya kuthibitisha makubaliano kuhusu biashara huria, kufanya majadiliano ya kina kuhusu sekta za biashara ya utoaji wa huduma na uwekezaji, na kupanua biashara huria katika sekta nyingi zaidi, ili kuhimiza mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani na uwekezaji wa biashara huria, na kujenga uchumi wa dunia ulio wazi kwa nje.

    Bw. Turnbull amepongeza juhudi za China katika kuhimiza utandawazi wa uchumi duniani, na kuhimiza ufunguaji zaidi wa soko kwa nje. Pia ameeleza kuwa anatumaini kushirikiana na China kukuza mawasiliano, kupanua ushirikiano ili kuhimiza nchi hizo mbili hata nchi zote duniani kupata amani na ustawi kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako