• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa mwito wa kuongeza uwezo wa ulinzi wa usalama wa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-24 17:54:10

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi jana ameitaka jumuiya ya kimataifa iunge mkono ujenzi wa jeshi la Afrika na vikosi vya dharura, ili kuongeza uwezo wa ulinzi wa usalama wa Afrika.

    Bw. Liu amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Somalia, ambapo limepitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

    Bw. Liu amesema China inaunga mkono Afrika itatue suala la Afrika kwa njia ya kiafrika, na kuuunga mkono Umoja wa Afrika na jumuiya nyingine za kikanda kuonesha umuhimu wa uongozi katika utatuzi wa masuala ya Afrika kwa njia ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako