• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Boao lafungwa kwa kutangaza mpango wa kuunga mkono utandawazi

    (GMT+08:00) 2017-03-27 09:05:03

    Mkutani wa baraza la uchumi la Boao la Asia umefungwa kisiwani Hainan kusini mwa China, na kutangaza mpango wa kuhimiza mafungamano ya kiuchumi.

    Lengo la mkutano wa baraza hilo lilikuwa ni kuhimiza na kuimarisha mafungamano ya kiuchumi, uratibu, ushirikiano ndani ya bara la Asia, na kati ya bara la Asia na sehemu nyingine za dunia. Ili kukabiliana na changamoto za ongezeko la uchumi na kupungua kwa mafungamano na kujilinda kibiashara, nchi za Asia zimekumbushwa kuendelea kuwa na masoko wazi, ongezeko shirikishi na ushirikiano wa kiuchumi.

    Pia imetajwa kuwa kujilinda kibiashara kunatakiwa kupingwa, na biashara na uwekezaji vinatakiwa kuhimizwa ili kusukuma mbele maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako