Benki Kuu ya Sudan na Wizara ya Madini imetangaza sera mpya za kununua na kuuza nje dhahabu.
Sera mpya, ambayo tayari imeanza kufanya kazi, itaruhusu sekta binafsi kuuza nje asilimia 50 ya dhahabu wanayonunua, na kuuza nusu nyingine kwa benki.
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Sudan, Hazem Abdelgadir alitangaza benki iko tayari kuanza kukubali maombi yoyote kutoka kwa makampuni, watu binafsi, na biashara ya kuuza nje dhahabu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |