• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalalamikia ziara ya waziri wa Japan huko Taiwan

    (GMT+08:00) 2017-03-27 21:10:05

    China imetoa malalamiko kwa Japan baada ya waziri mmoja wa nchi hiyo kufanya ziara huko Taiwan wikiendi iliyopita, ikisema hatua hiyo imekiuka ahadi yake katika suala la Taiwan.

    Naibu waziri wa mambo ya ndani na mawasiliano wa Japan Jiro Akama juzi alikwenda Taiwan kushiriki kwenye shughuli ya kutangaza utalii. Akama ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa serikali kufanya ziara rasmi huko Taiwan tangu Japan kuvunja uhusiano wake wa kibalozi na Taiwan mwaka 1972 na kuanzisha uhusiano huo na China.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Hua Chunying amesema hatua hiyo imekiuka dhahiri ahadi ya Japan ya kufanya mawasiliano yasiyo ya kiserikali na ngazi ya kanda na Taiwan, na ameongeza kuwa suala la Taiwan linahusu maslahi makuu ya China na haliwezi kujadiliwa.

    Habari nyingine zinasema vitabu vya shule ya sekondari ya juu nchini Japan vilivoidhinishwa Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia vimevitaja visiwa vya Diaoyu kuwa ni ardhi ya Japan. Bibi Hua amesema China inaitaka Japan iheshimu historia na hali halisi na kuacha kufanya uchochezi katika suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako