Kampuni ya ubia ya kutengeneza magari kati ya China na Zimbabwe jana ilizindua gari jipya aina ya Pickup, liitwalo "Grand Tiger" nchini Zimbabwe. Uzinduzi huo unafuatia Kampuni ya magari ya Beijing BAIC na kampuni mbili za Zimbabwe kushirikiana katika kuunda kampuni ya Beiqi Zimbabwe, itakayojihusisha na uagizaji, usambazaji na huduma za magari na vipuri, pamoja na usimamizi wa kifedha. Kampuni hiyo mpya inatarajiwa kutoa nafasi elfu tano za ajira na kuchangia kodi dola milioni 1.3 za kimarekani kwa mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |