• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Madagascar asema ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utawanufaisha wananchi wake

    (GMT+08:00) 2017-03-28 19:09:11

    Rais Hery Rajaonarimampianina wa Madagascar amesema, mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utakaofanyika mwezi Mei hapa Beijing utasaidia katika kutekeleza ujenzi wake, ambao pia utawanufaisha watu wa Madagascar.

    Rais Hery aliyeko ziarani nchini China amesema, Madagascar inaunga mkono pendekezo hilo ambalo limeonesha ufuatiliaji wa China kwa nchi za Afrika, na msimamo wazi wa China katika masuala ya amani, usalama na maendeleo duniani ambao ni kuondoa umaskini na kutimiza maendeleo yenye uwiano kati ya mabara tofauti ili kuhimiza mafungamano ya kiuchumi na maendeleo ya biashara huria duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako