• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNEP yasema sasa sio wakati wa kugeuza usukani juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:44:04

    Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Bw Eric Solheim amesema huu sio wakati wa kugeuza usukani juhudi za kukabiliana na tishio kubwa la mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw Solheim amesema uchunguzi wa kisayansi umeonyesha kuwa hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa. Amesisitiza kuwa matumizi ya nishati endelevu yenye kiwango cha chini cha kaboni ni njia sahihi ya kutimiza malengo ya kuwa na nishati safi yenye kutegemeka, ukuaji endelevu wa uchumi na kuleta nafasi nyingi bora za ajira.

    Rais Donald Trump wa Marekani jana alisaini agizo la kufuta sera za hali ya hewa zilizowekwa na rais wa zamani Barack Obama, ambalo pia linataka kuondoa ukomo wa utoaji wa hewa chafu viwandani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako