• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa na mauaji ya wataalam wawili wa Umoja huo nchini DRC

    (GMT+08:00) 2017-03-29 16:44:39

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vya wataalam wawili wa Umoja huo vilivyotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Katika taarifa yake, katibu mkuu huyo amethibitisha kuwa miili iliyopatikana March 27 na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) nje ya mji wa Kananga mkoani Kasai-Central, ni ya Michael Sharp raia wa Marekani na Zaida Catalan raia wa Sweden, ambao ni wajumbe wa Kundi la Wataalam kuhusu DRC waliopotea tangu tarehe 12 mwezi huu.

    Katibu mkuu huyo amesema, wawili hao wamepoteza maisha yao walipokuwa wakijaribu kutafuta sababu za migogoro na mapigano nchini DRC ili kusaidia kuleta amani katika nchi hiyo na watu wake.

    Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu hao, marafiki, na wapendwa wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako