• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza aahidi kutorudi nyuma baada ya kuanza mchakato wa Brexit

    (GMT+08:00) 2017-03-29 20:51:42

    Uingereza leo imeanza rasmi mchakato wa kihistoria wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, baada ya barua iliyosainiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Theresa May kupelekwa kwa viongozi wa Umoja huo.

    Akizungumza katika bunge la nchi hiyo, Bi. May amesema hatua hiyo ni ya kihistoria na hakuna kurudi nyuma, na kitakachofuata ni kuingia makubaliano ya kijasiri ya kibiashara na Umoja wa Ulaya.

    Hatua hiyo imekuja karibu miezi tisa baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye Umoja huo kwa asilimia 51.9 ya kura za ndio dhidi ya asilimia 48.1 za hapana katika kura ya maoni iliyopigwa majira ya joto mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako