• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liverpool kuvaana na Everton Aprili mosi

    (GMT+08:00) 2017-03-31 08:50:14

    Kivumbi kinatarajiwa kuruka jijini Liverpool wakati Liverpool itakapoialika Everton katika gozi la Merseyside uwanjani Anfield hapo kesho Aprili 1. Liverpool ya kocha Jurgen Klopp itakuwa mawindoni kudumisha rekodi ya kutoshindwa na Everton hadi mechi 12. Everton inayoongozwa na kocha Ronald Koeman, ambayo ushindi wake wa mwisho dhidi ya Liverpool ulikuwa 2-0 Oktoba 17 mwaka 2010, ilizabwa 4-0 kupitia mabao Divock Origi, Mamadou Sakho, Daniel Sturridge na Philippe Coutinho ilipozuru Anfield mara ya mwisho Aprili 20 mwaka 2016.Vijana wa Koeman watakuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Liverpool uwanjani Anfield tangu waliposhinda 1-0 Septemba 27 mwaka 1999.

    Liverpool na Everton zinashikilia nafasi za nne na saba kwenye msimamo wa ligi. Mchezaji anayeongoza katika kufunga mabao ligini msimu huu ni Romelu Lukaku wa Everton. Mbelgiji huyo, akiwa ameona lango mara 21, naye mfungaji bora wa Liverpool, Sadio Mane ana mabao 12. Kwingineko, mabingwa watetezi Leicester watatoana jasho na Stoke uwanjani King Power mnamo Aprili 1. Leicester iliyopo nafasi ya 15 iliipepeta Stoke 3-0 iliyopo nafasi ya tisa kupitia mabao ya Danny Drinkwater, Jamie Vardy na Leonardo Ulloa

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako