• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Clifton Miheso alalamika kwa FIFA kwa kusainishwa na Golden Arrows chini yam tutu wa bunduki

    (GMT+08:00) 2017-03-31 08:51:09

    Mchezaji wa kimataifa wa Kenya Clifton Miheso amewasilisha rasmi malalamiko katika shirikisho la soka duniani Fifa akidai kwamba alilazimishwa kwa mtutu wa bunduki kuhitimisha mkataba wake katika klabu ya Golden Arrows.

    Miheso anadai kisa hicho kilitokea Januari 14 katika afisi za klabu hiyo mjini Durban nchini Afrika Kusini. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 anataka Golden Arrows wapigwe marufuku kununua au kuuza wachezaji au wapewe adhabu nyingine yoyote ile.

    Aidha, anataka alipwe jumla ya $22,000 ambazo anasema anaidai klabu hiyo kama ujira wake. Golden Arrows wamekanusha tuhuma za mchezaji huyo lakini wakakataa kuzungumzia zaidi kisa hicho.

    Mwakilishi wa winga huyo anasema klabu hiyo haikutoa maelezo yoyote ya kuridhisha kuhusu kisa hicho. Miheso ameichezea timu ya taifa ya Kenya mechi 14 na kufunga magoli matano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako