• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yaidhinisha ujenzi wa makazi mapya kando ya magharibi ya Mto Jordan

    (GMT+08:00) 2017-03-31 18:36:46

    Baraza la Usalama la Israel limeidhinisha mpango wa ujenzi wa makazi mapya ya wayahudi katika kando ya magharibi ya Mto Jordan ili kupokea watu waliohamishwa kutoka eneo la Amona.

    Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Israel kuidhinisha ujenzi huo mpya katika Ukingo wa Magharibi katika miaka zaidi ya 20 iliyopita. Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema, waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu pia ametangaza kuidhinisha ujenzi wa nyumba nyingine mpya 2,000 katika eneo halali la makazi ya wayahudi. Pia amewaambia mawaziri kuwa ardhi yenye eneo la ekari 222 katika Ukingo wa Maghribi inayomilikiwa na Palestina itasajiliwa kama ardhi ya taifa la Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako