• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri mkuu wa Tanzania awaonya wakandarasi wasiomaliza kazi zao

    (GMT+08:00) 2017-03-31 19:59:42

    Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya nchi hiyo haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo na wanaoshindwa kuzimaliza kazi zao katika muda uliopangwa.

    Bwana Majaliwa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Chalinze na wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Chaliwasa) katika ofisi zao wilayani Bagamoyo,.

    Majaliwa amesema mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza majisafi pamoja na matangi ya kuhifadhia maji umechukua muda mrefu bila kukamilika.

    Awamu ya kwanza ilianza mwaka Septemba mosi 2001 na kukamilika Desemba mosi 2003.

    Majaliwa amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Bw. Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi wa mradi huo inaimarika na kufikia asilimia 80 la sivyo, wakamilishe taratibu za kukatisha mkataba na kutafuta mkandarasi mwingine.

    Agizo hilo linatokana na taarifa aliyopewa kwamba mkandarasi wa mradi huo, Overseas Infrastructure Alliance (OIA) Pvt Ltd ya India alipaswa kumaliza kazi hiyo Februari 22, mwaka huu lakini hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 23 pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako