• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanesco yaanza kuwakatia umeme wateja wake wanaodaiwa

    (GMT+08:00) 2017-03-31 20:00:31

    Hatua ya shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco la kuwakatia uememe wateja wake wanaodaiwa imeanza kuwaathiri wananchi. Taasisi na idara mbali mbali zinazotumia maji kutoka mamlaka ya maji safi na majitaka Bukoba ndizo zilizoathirika zaidi baada ya mamlaka hiyo kukatiwa umeme kufuatiwa deni la shilingi milioni 500.Kwa mujibu wa mtaalamu wa ufundi wa mamlaka hiyo Bw. Charles Chibuga , deni hilo linafaa kulipwa na wizara ya maji kwa mujibu wa makubaliano ya uendeshaji wa mradi huo. Hata hivyo kwa mujibu wa kaimu meneja wa Tanesco Bw Felix Olang amesema hatua hiyo ya kukata umeme inatokana na agizo la rais John Magufuli wa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako