• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu Tanzania Bara: Yanga yafuta historia mbaya ya kufungwa na Azam, huku Simba yavutwa shati Kagera.

    (GMT+08:00) 2017-04-03 08:22:19

    Yanga jumamosi ilifainikiwa kuifunga Azam FC goli 1-0 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Bao la yanga lilipatikana kunako dakika ya 70 ya mchezo huo kupitia kwa mchezaji wao wa kimataifa Obrey Chirwa baada ya kupokea pasi ndefu toka kwa Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kisha kumtoka beki wa Azam na hatimaye kukwamisha mpira kimiani.

    Ushindi huo umefuta historia mbaya ya Yanga kufungwa na Azam, tangu mwaka 2014, Yanga ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Azam. Kwa ushindi huo umezanza kurudisha matumaini ya Yanga kutetea ubingwa wao baada kujizolea pointi tatu na kufikisha pointi 56.

    Ligi hiyo imeendelea jana ambapo mahasimu na mtani wa jadi wa Yanga, Simba Sports Club kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako