• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali ya Uganda inakamilisha mipango yake ya kuondoa au kupunguza kodi kwa hoteli

    (GMT+08:00) 2017-04-03 19:48:10

    Serikali ya Uganda inakamilisha mipango yake ya kuondoa au kupunguza kodi kwa hoteli ili kuwawezesha wajasiriamali kuwekeza katika biashara ili kuvutia watalii zaidi, Waziri wa Utalii Efraimu Kamuntu amesema.

    Aidha hoteli nyingi nchini Uganda zimeshindwa kuboresha huduma zao kwa viwango vya kimataifa kwa sababu ya mzigo wa kodi.

    Aliongeza kuwa kuondolewa au kupunguzwa kodi matokeo yake yataonekana katika bajeti ya mwaka wa 2017/18.

    Serikali inataka kuongeza idadi ya watalii ambao huja Uganda kila mwaka milioni 1.3 hadi milioni 4 ifikapo mwaka wa 2020.

    Prof Kamuntu amebaini kuwa sekta ya utalii kwa sasa inachangia asilimia 9 kwa pato la taifa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako