• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serengeti Boys yalazimisha sare kwa Ghana.

    (GMT+08:00) 2017-04-04 08:34:59

    Timu ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Ghana katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya jana.

    Huo ulikuwa mchezo wa tatu wa majaribio katika maandalizi ya Serengeti Boys kwenda Gabon kwenye fainali za Afrika za U-17 mwezi Mei baada ya awali kuifunga Burundi 3-0 na 2-0 mjini Bukoba wiki iliyopita.

    Ghana walitangulia kwa mabao mawili ya Sulley Ibrahimu dakika ya 30 na Arko Mensah dakika ya 73, kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Asad Juma kwa penalti na Muhsin Malima mabao yote yakifungwa dakika za nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako