• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wazidi kuwika katika Marathoni Duniani.

    (GMT+08:00) 2017-04-04 08:36:08
    Kenya imeendeleza ubabe wake katika mbio za Milano Marathon jijini Milan nchini Italia baada ya Edwin Koech na Sheila Chepkoech kuibuka washindi Aprili 2, 2017.

    Koech sasa anamiliki muda wa kasi ya juu kuwahi kutimkwa nchini Italia. Ameshinda mbio hizo za kilomita 42 kwa saa 2:07:13. Alifuta rekodi ya Mkenya mwenzake Benjamin Kiptoo, ambaye alinyakua taji la Rome Marathon mwaka 2009 kwa saa 2:07:17.

    Na kwa upande wa akina dada, Chepkoech ameshangaza wengi alipoibuka bingwa wa Milano Marathon kwa saa 2:29:52, kasi ambayo ni zaidi ya dakika 10 ya muda wake bora.

    Nafasi ya nne kwa upande wa wanaume imeshikiliwa na Muethiopia Abdela Godana na nafasi ya mwisho imekamatwa na YaSINE Rachik wa Italia. Kwa wanawake, Anna Incerti wa Italia ameshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa Waka Chaitu wa Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako