• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsene Wenger asema si rahisi kutinga nne katika ligi

    (GMT+08:00) 2017-04-05 08:26:53

    Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kushindwa kwa timu yake kufanya vizuri msimu huu kunamaanisha kwamba sio rahisi kwa timu hiyo kuwa katika orodha ya timu nne bora msimu huu.

    Wenger ambaye ni raia wa Ufaransa ameongoza The Gunners katika nafasi nne bora katika kombe la vilabu bingwa kwa miaka 20 iliyopita.

    Lakini ikiwa imesalia mechi 10, Arsenal iko katika nafasi ya sita ikiwa nyuma ya timu nne zinaozoongoza ligi hiyo.

    Wenger amesisitiza kuwa ni changamoto kubwa kuwa katika nafasi nne bora lakini anaona inawezekana.

    Mwaka 2012 Wenger alisema timu ikiwa miongoni mwa nafasi nne bora ni sawa na kushinda taji, maoni ambayo yaliungwa mkono na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako