• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serengeti Boys yaelekea kambini nchini Morocco

    (GMT+08:00) 2017-04-06 08:51:14

    Kikosi cha wachezaji 23 cha Serengeti Boys pamoja na viongozi kimeondoka jana kuelekea nchini Morocco kwaajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana huku kikiahidi kuitumia kambi hiyo ili kurudisha matumaini Tanzania. Kocha wa timu hiyo Bakari Shime amesema, kikosi chote kipo imara kisaikolojia na anaamini watalipa deni la watanzania kwa kuitumia kambi hiyo vizuri ili kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya AFCON nchini Gabon.

    Shime amesema, mpaka sasa wamebakiza mechi takribani nne za kirafiki ili kuhakikisha kikosi kinakuwa imara kwa ajili ya kwenda kupambana nchini Gabon. Kwa upande wake nahodha wa kikosi hicho. Issa Abdi Makame amewataka watanzania kuendelea kuwachangia ili kuongeza morali ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Mei 14 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako