• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya kodi ya Tanzania TRA yaendelea kutikisa soka kwa madai ya kodi

    (GMT+08:00) 2017-04-07 09:18:27

    WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dk Harrison Mwakyembe amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na kampuni ya udalali ya Yono kuwashusha kwenye basi wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kutokana na deni wanalodaiwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mamlaka ya Mapato (TRA).

    Tukio la Yono kuwashusha Serengeti Boys kwenye basi na kuondoka nalo, lilitokea Dar es Salaam wakati timu hiyo ikiwa kwenye basi hilo tayari kwa safari ya kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliyewaalika kwa chakula cha jioni kuwaaga kwa safari ya kwenda Gabon kwenye michuano ya Afrik,a ambapo wataanzia Morocco kwenye kambi ya maandalizi. Kwa muda mrefu, TRA imekuwa kwenye malumbano ya kodi na TFF ikiwadai malimbikizo ya kodi Sh bilioni 1.2 kama kodi za mishahara ya waliokuwa makocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo na Mdenmark, Jan Poulsen kwa miaka takriban minane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako