• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu ya Chelsea ya Uingereza yataka kumsajili Lukaku

    (GMT+08:00) 2017-04-07 09:19:51

    Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea wako mbioni kunasa saini za mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku na beki wa AS Roma, Antonio Rudiger.

    Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye anataka kumrudisha Lukaku mwishoni mwa msimu huu baada ya staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuuzwa na Jose Mourinho katika dirisha kubwa la majira ya joto 2014.

    Katika hatua nyingine Conte akiendelea kumuwinda staa AS Roma, Antonio Rudiger wakati wa pambano la Kombe la Italia dhidi ya wapinzani wao wa jadi Lazio. Tayari maskauti wa Chelsea walishamtazama staa huyo katika pambano la kirafiki kati ya Ujerumani dhidi ya England mwezi uliopita jijini Dortmund na Conte anataka kumfanya Rudiger kuwa mbadala wa muda mrefu wa mkongwe, John Terry.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako