• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania washauriwa kutotumia mafuta hafifu

    (GMT+08:00) 2017-04-07 19:19:11

    Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka Watanzania wasikubali kuendelea kupata hasara kwa kutumia petroli na mafuta yaliyo hafifu, kwa kuwa mashine ya kupima ubora wa mafuta hayo na mazao yake ipo kwa ajili ya kuwathibitishia kama yanafaa kwa matumizi au la.

    Shirika hilo pia limetoa mwito kwa wamiliki au watumiaji wa magari na mitambo wanaoharibikiwa na vifaa vyao kwa sababu ya kutumia mafuta wanayoamini kuwa hayana ubora unaotakiwa, wafikishe sampuli za mafuta hayo TBS ili zipimwe kuona kama kuna tatizo, badala ya kuwafuata waliowauzia bila ushahidi wa kimaandishi.

    Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Viwango katika maabara ya mafuta ya TBS, Charles Batakanwa amesema mtambo wa kisasa wa kupima ubora wa mafuta ya petroli, dizeli, vilainishi vya mitambo na magari, gesi na mazao yote ya petroli yakiwemo mafuta ya kupaka upo katika shirika hilo, lakini watu binafsi hawautumii.

    Kwa mujibu wa Batakanwa, shirika linatambua kuwa wapo watu wanaoendelea kupata hasara kwa kutumia mafuta hafifu, lakini hawajitokezi kuthibitisha wanayoyatilia mashaka, badala yake wanalalamika chini chini kwa kuharibikiwa na mitambo au magari na kupata hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako