• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa mahindi walalamikia hatua ya serikali ya Kenya kuagiza mahindi kutoka nje

    (GMT+08:00) 2017-04-07 19:19:43

    Wakulima wa mahindi nchini Kenya wamepinga mpango wa serikali wa kuruhusu uagizaji wa mahindi yasiyotozwa ushuru kwa ajili ya kupunguza bei ya unga.Wakulima hao wamesema mpango huo ni wa maafisa fulani wenye ushawishi mkubwa serikalini kwa ushirikiano na wasagaji na wanalenga kuchuma faida kubwa kutokana na biashara ya mahindi huku wakiumia kwa kukosa soko la zao hilo msimu huu. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa muungano wa wakulima Bw Kipkorir Arap Menjo, serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa idadi ya magunia ya mahindi yatakayoagizwa haizidi idadi ya magunia yanayokadiriwa kupatikana katika msimu huu. Uagizaji wa mahindi unafaa kudhibitiwa ili kuzuia kushuka kwa bei ya zao hilo na kuwaathiri wakulima . Kauli hiyo inakuja wiki moja tui baada ya serikali kutoa magunia milioni moja ya mahindi kwa wasagaji kwa lengo la kushukisha bei ya unga wa mahindi ambao umepanda hadi kufikia shilingi 150 kwa pakiti ya kilo mbili. Serikali inapanga kuagiza mahindi kutoka Ethiopia, Mexico kwa bei rahisi ya shilingi elfu 2 kwa gunia la kilo 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako