• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Barafu inayoyeyuka katika ncha ya kaskazini ya dunia inawapatia viumbe wa baharini lishe nyingi

  (GMT+08:00) 2017-04-10 16:45:48

  Watafiti wa Denmark wamegundua kuwa kuyeyuka kwa barafu katika ncha ya kaskazini ya dunia kunaweza kuwanufaisha viumbe vya habarini, kwani lishe nyingi kwenye barafu zinaingia baharini, na kuifanya bahari iwe na chakula kingi zaidi.

  Mwandishi wa kwanza wa ripoti ya utafiti ambaye pia ni mtafiti wa Chuo Kikuu cha Denmark Kusini alisema baada ya barafu kuyeyuka, mwani na viumbe vingine mbalimbali vinaingia baharini.

  Na si kama tu viumbe wanaoishi kwenye sehemu ya juu ya bahari wanapata chakula kingi zaidi, viumbe wanaoishi kwenye kina kirefu pia watanufaika. Ingawa viumbe wa sehemu ya juu wanakula mara moja chakula wanaochopata, lakini bado kuna vyakula vingine vinavyoanguka chini ya bahari na kuliwa na viumbe wa huko.

  Wanasayansi wamechunguza uyeyukaji wa barafu katika ncha ya kaskazini katika miongo kadhaa iliyopita, na kugundua kuwa viumbe vidogo vidogo vinaweza kuishi kwenye maziwa yanayotokea baada ya barafu kuyeyuka, lakini hawajui kwa nini viumbe havikuwepo kwenye baadhi ya maziwa. Utafiti mpya umepata jibu la swali hili, kwamba lishe mbalimbali zikiwemo Phosphorus na Nitrogen ambazo ni muhimu kwa maisha ya viumbe zinapelekwa maziwani kupitia mawimbi na ndege, lakini si maziwa yote yanayoweza kufikiwa na lishe hizi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako