• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juventus yaizamisha Barcelona kwa 3-0

    (GMT+08:00) 2017-04-12 09:53:14
    Baada ya mapumziko mafupi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya Juventus dhidi na FC Barcelona ulichezwa mjini Turin wakati mchezo wa Borussia Dortmund dhidi ya Monaco ukiahirishwa hadi April 12 kwa sababu za kiusalama.

    Mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Juventus nchini Italia ulianza kuibeba Juventus kuwa na rekodi ya kutowahi kufungwa na Barcelona katika ardhi ya Italia, wakiwa wamewahi kutoka sare mara mbili na Barcelona na kupoteza mara mbili wakati mara ya mwisho kukutana ilikuwa Berlin katika mchezo wa fainali UEFA Champions League 2015 na Juventus akapoteza kwa magoli 3-1.

    Katika mechi hii Juventus wakiwa Turin wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yakifungwa na Paulo Dybala dakika ya 7 na 22 na goli la mwisho likafungwa na Giorgio Chiellini dakika ya 55. Barcelona walicheza kufa na kupona kujaribu kupata japo bao moja la ugenini lakini hawakuweza kufua dafu. Juventus na Barcelona watacheza mchezo wa marudiano April 19 Nou Camp.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako