• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KRC Genk yapokea kichapo cha magoli 3-2

    (GMT+08:00) 2017-04-14 08:40:17
    Timu ya KRC Genk jana iliingia uwanjani kucheza mechi yake ya Europa League dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wa Balaidos Hispania.

    Mchezo huo ulikuwa ni robo fainali ya kwanza na KRC Genk waliokuwa ugenini wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza baada ya kucheza mingine sita mfululizo bila kupoteza katika mashindano yote. Genk wamefungwa magoli 3-2, katika historia Genk na Celta Vigo ndio wamekutana kwa mara ya kwanza.

    Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffel aliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38, kipigo hicho kinailazimu Genk katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Luminus Arena April 20 wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu nusu fainali.

    Kwa upande wa Mbwana Samatta amecheza mechi hiyo kwa dakika zote 90 na kutimiza jumla ya dakika 756 alizocheza katika mechi zote 11, akifunga magoli mawili, usaidizi mara moja na akipiga jumla ya mashuti 7 yaliyolenga goli, Samatta baada ya kufunga katika mechi 5 mfululizo za Genk jana amecheza game yake ya pili bila kufunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako