• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya saa 72 yaipa Simba pointi zote tatu dhidi ya Kagera Sugar

    (GMT+08:00) 2017-04-14 08:40:46
    Kamati ya saa 72 ilikaa kikao chake jana na kuamua kuhusu malalamiko ya Simba kwa Kagera Sugar kuhusu kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi katika mchezo dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano kinyume na taratibu na kanuni za Ligi.

    Simba walipeleka malalamiko hayo katika bodi ya Ligi na kuomba ipitie ripoti za waamuzi ili kujulikana ukweli, kamati ya saa 72 chini ya mwenyekiti wake Hamadi Yahaya ilikaa na kujiridhisha kuwa Kagera walikiuka taratibu hizo kwa mujibu wa Kanuni Simba wamepewa point zote tatu za mchezo dhidi yao.

    Kamati imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alioneshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Majimaji, Mbeya City na African Lyon, hivyo hakustahili kucheza katika mchezo dhidi ya Simba uliyochezwa April 2 2017 uwanja wa Kaitaba na Simba ikapoteza kwa magoli 2-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako