• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Didier Drogba ajiunga na klabu ya ligi daraja la kwanza ya Marekani Phoenix Rising

    (GMT+08:00) 2017-04-14 08:41:12
    Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast Didier Drogba amejiunga na klabu ya ligi daraja la kwanza ya Marekani Phoenix Rising kama mchezaji na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo. Drogba mwenye umri wa miaka 39, hakucheza soka tangu aachane na klabu ya ligi kuu ya soka nchini Marekani Montreal Impact mwaka uliopita.

    Taarifa ya klabu ilisema mshambuliaji huyo mkongwe Didier Drogba amejiunga na uwekezaji wa ligi kuu ya soka ya Marekani, na atawekeza zaidi kwa mafanikio ya klabu ya ligi daraja la kwanza.

    Kwa upande wake Drogba alisema kumiliki timu na kuwa mchezaji kwa wakati mmoja siyo kitu cha kawaida, lakini kwake yeye ni kitu cha kusisimua. Drogba alifunga mabao 157 katika mechi 341 alizochezea Chelsea katika kipindi cha 2004 hadi 2012, akishinda mataji matatu ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza na taji moja la ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako