• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 36 wa kundi la IS wauawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na Marekani nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-04-14 18:36:39

    Wapiganaji 36 wa kundi la IS wameuawa mashariki mwa mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan baada ya vikosi vya Marekani kushambulia maeneo yao kwa bomu kubwa.

    Jana jioni, vikosi vya Marekani vilidondosha bomu aina ya GBU-43, ambalo ni bomu kubwa zaidi lisilo la nyuklia, katika eneo la kundi la IS wilayani Achin, mkoa wa Nangarhar unaopakana na Pakistan. Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, hakuna raia waliouawa katika shambulizi hilo ambalo liliharibu makao makuu ya kundi hilo, sehemu tatu za maficho ya wapiganaji wa kundi hilo, pamona na kiasi kikubwa cha silaha na risasi.

    Habari nyingine zinasema, shambulizi lingine lililofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Syria limesababisha vifo vya wapiganaji 18 wa kundi la IS nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako