• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajimu wa Uingereza wagundua "doa kubwa baridi" kwenye sayari ya Jupiter

    (GMT+08:00) 2017-04-14 18:48:02

    Hivi karibuni wanajimu wa Uingereza wamegundua kimbunga kikubwa cha pili kwenye sayari ya Jupiter baada ya kimbunga cha "doa kubwa Jekundu", na kimbunga hiki kipya kimepewa jina la "doa kubwa baridi".

    Kikundi cha watafiti kinachoongozwa na Uingereza kimegundua kimbunga hiki chenye urefu wa kilomita elfu 24 na upana wa kilomita elfu 12. Kiko kwenye sehemu ya juu ya hewa ya sayari hiyo, na baridi zaidi kuliko hewa iliyoko kando yake. Kimbunga hiki kiliundwa kutokana na nishati ya mwanga wa Aurora kwenye ncha ya sayari hii, na bado kinaendelea kubadilika.

    Kikundi cha Watafiti kilirekodi joto na uzito wa hewa ya Jupiter kwa darubini iliyoko nchini Chile, na kulinganisha data na picha mpya na zile zilizorekodiwa na darubini iliyoko Hawaii, Marekani katika miaka mingi iliyopita, na mwishowe kugundua kimbunga hiki chenye historia zaidi ya miaka elfu moja.

    Kimbunga kingine kikubwa zaidi cha "doa kubwa jekundu" ambacho kiligunduliwa na wanasayansi miaka 150 iliyopita kinajulikana na watu wengi zaidi, ambacho kina urefu wa kilomita elfu 25 na upana wa kilomita elfu 12.

    Dr. Tom Stallard kutoka Chuo Kikuu cha Leicester cha Uingereza ambaye ni mwandishi wa kwanza wa tasnifu alisema "doa kubwa baridi" hakitulii sana kikilinganishwa na "doa kubwa jekundu" ambacho kinabadilika polepole.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako