• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mali ya mameneja wa benki ya Chase yakamatwa

    (GMT+08:00) 2017-04-14 20:12:59

    Mahakama kuu ya Kenya imeagiza kukamatwa kwa mali za mameneja wa zamani wa benki ya Chase ikisema mali hiyo ilinunuliwa kwa fedha za benki hiyo zilizochukuliwa kwa njia ya udanganyifu. Jaji wa mahakama kuu Fred Ochieng ametaka mali za mameneja hao kutouzwa au kuhamishiwa watu wenghine hadi pale mahakama itakapotoa hukumu yake. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakama ilifahamishwa kuwa taarifa za fedha za benki hiyo zinaonesha kuwa Disemba 31 mwaka wa 2015 kulikuwa na uporaji mkubwa kwenye benki hiyo. Aidha mahakama pia ilifahamishwa kuwa mameneja hao walifungua makampuni ya kitaifa na kimataifa ambayo walitumia kufanya uporaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako