• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maofisa 28 wa ATCL kwenda Ethiopia kwa mafunzo zaidi

  (GMT+08:00) 2017-04-14 20:13:14

  Maofisa 28 wakiwemo marubani 10 wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) wanatarajia kwenda kupata mafunzo ya urubani nchini Ethiopia baada ya makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukamilika, ikiwa ni manufaa ya ziara ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.

  Aidha, Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa kampuni hiyo, Kapteni Richard Shaibu anatarajiwa kuondoka mwisho wa mwezi huu kwenda Ethiopia kwa ajili ya kuhakikisha makubaliano yaliyowekwa na viongozi wakuu wa nchi hizo yanatekelezwa.

  Akizungumza na wawakilishi wa Shirika la Ndege la Ethiopia ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema kwa sasa wako katika hatua ya kuhakikisha makubaliano yaliyowekwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Desalegn hivi karibuni yanatuimia.

  Matindi alisema wamekubaliana kuwa mwishoni mwa Mei au mwanzoni mwa Juni, baadhi ya marubani na wahandisi wataanza kwenda kwenye mafunzo, ambayo wahandisi ni 18 na marubani 10 ambao wataanza mafunzo ya mwanzo, lakini kutakuwa na mafunzo ya mara kwa mara kuhakikisha wanakuwa katika viwango vinavyotakiwa.Alisema ahadi nyingine ya Waziri Mkuu Desalegn ni kuanzisha kituo kikubwa Afrika cha kuhudumia mizigo nchini na kuleta wataalamu watakaosaidia kuijengea uwezo ATCL wa kushindana na kufanya biashara na kupata faida.

  Pia alisema watashirikiana katika tiketi za ndege kwa kuwa Ethiopia iko karibu hivyo wataokoa gharama za usafiri

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako